Total Pageviews

Thursday, January 21, 2016

JIFUNZE KUTENGENEZA PIPI ZA KIHINDI ,UONGEZE KIPATO CHAKO.


Sukari  Guru  ya  njano. Moja  kati  ya  malighafi  inayo  tumika  kutengeneza  pipi  za  kihindi.


·       Wewe  ni  kijana  wa  kitanzania ?
·       Unataka  kuongeza  kipato  chako ?
Kama  jibu  lako  ni NDIO  basi   hii  ni  HABARI NJEMA  SANA  KWAKO. Taasisi  ya  NEEMA  INSTITUTE  OF  N.G.O  MANAGEMENT  kupitia MRADI  WA  UANZISHAJI, UENDESHAJI  NA USIMAMIZI  WA BIASHARA  NDOGONDOGO  inatangaza  nafasi  za  kushiriki  katika  SEMINA  YA  UJASIRIAMALI.   Somo  litakalo fundishwa  ni

 UTENGENEZAJI  WA  PIPI  ZA  KIHINDI.

Pipi  za  Kihindi  ni  bidhaa  inayo  pendwa  sana  na  watoto  wa  shule  ya  msingi  na  hata  sekondari.
Washiriki  katika  Semina  hii, watapewa nafasi  za  biashara  katika  shule mbalimbali  za  msingi  zilizopo  jijini  Dar  Es  Salaam.

Sukari  Guru.


ADA  YA  KUSHIRIKI  KATIKA  SEMINA  HII    NI  SHILINGI  ELFU   HAMSINI    TU (Tshs.50,000/=)

Fomu  za  kujiunga  katika  semina  hii, zinapatikana  ofisini  kwetu  kwa gharama  ya  Shilingi  ELFU  KUMI  NA  TANO  TU
( Tshs.15,000/=).

Tunapatikana  UBUNGO   Dar  Es  Salaam, jirani  na  Shule  Ya  Msingi  Ubungo  National  Housing  nyuma  ya  jengo  la  Ubungo  Plaza.

Mwisho  wa  kuchukua  fomu  ni  tarehe  30  JANUARY 2016  saa  nane  kamili  mchana.

Semina   itafanyika  kwa  siku  tano,  kuanzia  tarehe  01  Februari 2016  hadi  tarehe  05  February 2016.

Kwa  maelezo  zaidi  kuhusu  semina  hii , wasiliana  nasi  kwa  simu  namba  0766  53  83  84    AU   Tembelea  blogu  yetu :===============================================FAIDA   ZA  KUSHIRIKI  KWENYE  SEMINA  KUHUSU  MAFUNZO  YA  UTENGENEZAJI WA  PIPI  ZA  KIHINDI.


Sukari  Guru  ya  Brown

  
Taasisi   ya  Neema  Institute  Of  N.G.O  Management  yenye  ofisi  zake  jijini  Dar  Es  Salaam, katika  eneo  la  Ubungo  imeandaa    SEMINA  KUHUSU   UTENGENEZAJI  WA  PIPI   ZA  KIHINDI  ambayo  itafanyika  kwa  muda  wa  siku  tano, kuanzia  tarehe  01  FEBRUARY  2016  hadi  tarehe  05 FEBRUARI 2016.

Lengo  la  semina  hii  ni  kuwasaidia  wajasiriamali  wadogo  wadogo  na  wale  wa  kati, kupata  ujuzi  utakao  wasaidia  kuongeza  vipato  vyao.

Zifuatazo  ni   faida   za  kushiriki  katika  semina  hii:

1.     Mafunzo  yanafundishwa  kwa  njia  ya  nadharia  na  vitendo  ( Theory  and  Practical )kila  siku  kwa  siku  zote  tano  za  mafunzo .  Katika  siku  zote  tano  utakazo  hudhuria  mafunzo  haya, utapata  kujifunza  kwa  vitendo  jinsi  ya  kutengeneza  pipi  za  kihindi. Lengo  letu  ni  kuhakikisha  kila  anaye shiriki  katika  semina  hii, anatoka  akiwa  amewiva  katika  suala  zima  la  utengenezaji  wa  pipi.

2.     NI    BIDHAA  YENYE  SOKO  LA  UHAKIKA :

Pipi   za  kihindi  ni  pipi  zinazo  tengenezwa  kwa  kutumia  malighafi  iitwayo   sukari  guru  pamoja  na   viambatano  (ingredients )  vingine .   Pipi  hizi  ni  bidhaa  inayo pendwa  sana  na  watoto  wanao  soma  katika  shule  za  msingi  na  sekondari .  Kwa  muda  mrefu sasa, wahindi  wanajulikana  dunia  nzima  kwa  kuwa   na  umahiri  mkubwa  wa  kutengeneza   vitu  vitamu  tamu pamoja  na  vyakula  vizuri  kwa  ujumla.  Hivyo  basi  suala  la  pipi  za  kihindi.
 
Utafiti  wetu  umetuwezesha  kugundua, kwa  biashara  ya  kuuza  pipi  za  kihindi   mashuleni, unaweza  kuingiza  faida  ya  kati  ya  shilingi  Elfu Thelathini  ( Tshs.30,000/=)  hadi   Shilingi  Elfu  Themanini  (Tshs.80,000/=)  kwa siku, kutegemeana  na  kiwango  cha  uzalishaji  wako.
 Na  kama  utapata  nafasi  katika  shule  zaidi  ya  moja, kipato  chako  kitakuwa  kikubwa  maradufu.

3.     UHAKIKA  WA  KUPATA  NAFASI  YA  BIASHARA  KWENYE  SOKO  LA  UHAKIKA .
Baada  ya  kuhitimu  mafunzo,  kila  mshiriki, atapewa  nafasi  ya  biashara    katika  shule  ya  msingi  yenye  idadi  kubwa  ya  wanafunzi 
iliyopo  jijini  Dar  Es  Salaam  na  hivyo  kumuwezesha  kutengeneza  kipato  cha  uhakika, kupitia  biashara  ya  pipi za  kihindi. Sisi  kama  Taasisi  tunazo  nafasi  zaidi ya  mia ( 100 ) katika  shule  mbalimbali  za  msingi  zilizopo  jijini  Dar  Es  Salaam zenye  idadi  ya  wanafunzi  kati  ya  mia  nne  (400)  hadi  elfu  moja  (1000).
Nafasi  hizi  za  biashara  tutazitoa  kwa   watakao  hitimu  mafunzo  yetu.
Nafasi  hii  utaipata  baada  ya  kumaliza  mafunzo. Mafunzo  yanaanza  Jumatatu na  kuisha  Ijumaa. Siku  hiyo  hiyo  ya  Ijumaa  unapewa  details  za  shule  utakayo  enda  kufanyia  biashara  yako, Jumamosi  na  Jumapili, unazitumia  kufanya  maandalizi  ya  kutengeneza  pipi  zako, na  Jumatatu  unaanza  kuingiza  pesa  kupitia  shughuli  ya  kuuza  pipi  kwenye  shule  ambayo  tutakuwa  tumekupangia.

(  FURSA  YA  KUPATA  NAFASI  YA  BIASHARA  INAWAHUSU  WALIOPO  DAR  ES  SALAAM  TU  )

4.     MTAJI  MDOGO  WA  BIASHARA :  Mradi  wa  kutengeneza  na  kuuza  pipi za kihindi  mashuleni, hauhitaji kiasi  kikubwa  cha  fedha  za  mtaji. Hata  kwa  wajasiriamali  ambao  ndio  kwanza  wanaanza  ujasiriamali na  hawana uwezo mkubwa wa  kifedha  wanaweza  kumudu.


5.     UTAPATA  FURSA  YA  KUUNGANISHWA  NA  WAJASIRIAMALI  WENZAKO  NA  KUUNDA  TAASISI  ISIYO  KUWA  YA  KISERIKALI.

Washiriki  wa  mafunzo  haya, wataunganishwa  pamoja  na  kuunda  Taasisi  isiyo  kuwa  ya  kiserikali ( N.G.O ), ambapo  wata saidiwa  kuanzisha  VICOBA  pamoja  na  kufundishwa  utengenezaji  wa  bidhaa  nyinginezo  zinazo  pendwa  sana  na  watoto  mashuleni  kama  vile  Ubuyu  wa  Zanzibar  nakadhalika.


6.      SEMINA  INATOLEWA  KWA  MUDA  AMBAO  HAUWEZI KUHARIBU  RATIBA  YAKO.
Kutakuwa  na  madarasa  ya  asubuhi  pamoja  na  madarasa  ya  jioni. Madarasa  ya  asubuhi  yanaanza  saa  nne  hadi  saa  sita. Na  madarasa  ya  jioni  yanaanza  saa  kumi  hadi  saa kumi  na  mbili  Hivyo  basi  kama  wewe  ni  muajiriwa  na   hauna  nafasi  muda  wa  asubuhi, unaweza  kupata  fursa  ya  kushiriki  katika  semina hii wakati  wa   jioni  kuanzia  saa  kumi  hadi  saa  kumi  na  mbili.

7.      UNAWEZA KUJIFUNZA  KUTENGENEZA  PIPI  ZA  KIHINDI  NA  UKAAJIRI  VIJANA WENGI  WA  KAZI  NA  KUTENGENEZA  FEDHA  MARADUFU.

Unaweza  kujifunza  kutengeneza  pipi  hizi, halafu  ukatafuta  nafasi  ya  biashara  kwenye  shule  mbalimbali  za  msingi   na  kuwaweka  vijana  wa kazi.   Ukipata  nafasi  katika  shule  nyingi, maana  yake  hata  kipato  chako  kitaongezeka  mara  dufu.


Hizo  ni  baadhi  ya  faida  za  kushiriki  katika  mafunzo  haya.


KWA   WALIOPO   NJE   YA  MKOA  WA  DAR  ES  SALAAM.
Kwa  waliopo  nje  ya  mkoa  wa  Dar  Es  Salaam, mafunzo   haya yatatolewa  kwa  njia  ya  Posta. Utapatiwa  DVD  na  VITABU  vinavyo  elezea  STEP  by  STEP  kuhusu namna  ya  KUTENGENEZA  PIPI  ZA KIHINDI.

JINSI   YA  KUJIUNGA  NA  MAFUNZO  HAYA  KWA  WAOMBAJI  KUTOKA  NJE  YA  DAR  ES  SALAAM.
Kama  upo  nje  ya  mkoa  wa  Dar  Es  Salaam, na  unataka  kushiriki  katika  mafunzo  haya, tuandikie  barua  pepe  ya  maombi  ya  kushiriki  katika  mafunzo  haya. Barua  pepe  yetu  ni :  neemainstitute@gmail.com
Mwisho  wa  kupokea  maombi  ni  tarehe  30 JANUARY  2016.EWE  MZAZI !  EWE  MLEZI ! UNA NGOJA  NINI ?
MLETE  KIJANA  WAKO  APATE   MAFUNZO  YATAKAYO  MSAIDIA   KUINGIZA  KIPATO  CHAKE.

EWE  KIJANA!  ZAMA  ZA  KUAJIRIWA  ZIMEPITWA  NA  WAKATI. USISUBIRI  KUAJIRIWA.  NJOO  UPATE  UJUZI  UTAKAO  KUSAIDIA  KUINGIZA  KIPATO KIZURI

Tuesday, December 29, 2015

Mwanamuziki K.Michele afanya operation kupunguza ukubwa wa makalio

K. Michelle gets butt reduction ...shares photos of her new size

Singer K. Michelle said she was going to reduce her butt implant because it was taking attention away from her and her talent, and she's started the process. She's had her first booty reduction surgical procedure and reportedly removed a gallon of fat from her butt. She will remove more. She shared photos of the size of her new butt. Read what she wrote and more photos after the cut...


Thursday, December 24, 2015

APOPO : Shirika linalofunza panya kunusa na kutafuta mabomu ya kutegwa ardhinika


Shirika linalofunza panya kunusa na kutafuta mabomu ya kutegwa ardhini limetuma picha hizi za panya wakiwa wamevaa kofia za 'Father Christmas' kusherekea Krismasi. Panya hawa wanapewa mafunzo na shirika la Apopo mkoani Morogoro nchini Tanzania, na hutumika kusaka mabomu ya kutegwa 
ardhini nchini Angola na Msumbiji.
Pics: See the luxury resort where Obama will spend his Christmas vacation


The Hale Reena in Kailua, Hawaii, dubbed the other White House is the vacation home of Obama and his family in what will be their eighth consecutive Christmas vacation to Hawaii and at $3500-a-night, it doesn't come cheap. Amenities include a spa, pool, steam room and excellent out door facilities. See more photos after the cut...

President Obama will be paying the rent out of his pocket but other expenses such as security and the daily expenses of his security detail will be picked up by the taxpayer. The first family first stayed at the Hale Reena in 2011 when their usual first choice, The Plantation Estate wasn't available, that can cost between $5000-$10000 a night depending on the season.

Monday, December 21, 2015

KILIMO BORA CHA MDALASINI - CINNAMON


.

Mti wa mita 10 au zaidi. Hutoa machipukizi na kuota miti zaidi ya mmoja kwenye shina moja na kuongeza mavuno mengi, haya mashina mapya yasing'olewe bali yaachwe yakue na kuwa mti mkubwa

AINA
Mchanganyiko; za kienyeji (ndogo) na za kigeni ( kubwa)

HALI YA HEWA NA UDONGO
· Mvua nyingi za kutosha 2000mm -2500mm kwa mwaka
· Udongo wenye rutuba
· Joto kwa wingi
· Hewa yenye unyevunyevu

KUSIA MBEGU KWENYE VITALU
· Mbegu hupatikana kwenye miti iliyokomaa
· Sia mbegu kwenye kitalu zikiwa nusu sentimeta chini ya udongo
· Baada ya kuchipua, mbegu huchukua miezi 6 hadi mwaka mmoja kufikia umri wa kupandikiza shambani
· Panda miche wakati wa masika
· Panda kwa nafasi ya 2m x2m. Nafasi hizi huwezesha miti kutoa machipukizi mengi. Nafasi kubwa hufanya miti kuwa na matawi mengi pia mashina hayanenepi wala kurefuka

UTUNZAJI
· Acha machipukizi kwenye shina
· Toa matawi kwenye mashina ili kunenepesha mashina
· Weka shamba katika hali ya safi
· Zuia magonjwa kama.
- Vinundu (galls)wanaosababishwa na utitiri na wadudu scales na mealbugs kwa kutumia dawa za sumu kama Selecron, Karate nk.

KUVUNA
· Anza kuvuna miaka 3 baada ya kupanda
· Mazao ya mdalasini ni maganda ya mashina ya miti
· Kata shina la mti,na tenganisha maganda na mti kwa njia ya kumenya
· Kuwa mwangalifu ili ganda litoke vizuri bila kupasukapasuka
· Seli za nje ya ganda la mdalasini ni chungu hivyo ni vizuri ziondolewe kwa kukaruza kwa kisu
· Kausha vizuri siyo kwenye jua kali Mavuno
· 0.25 kg – 10kg maganda yaliyokaushwa kwa mti mmoja. Kiasi cha mazao hutegemea ukubwa na umri wa mti
· Ubora wa mdalasini hushuka kulingana na umri wa mti. Mti wa umri mkubwa hutoa mganda yenye ubora wa chini

MATUMIZI
Mdalasini baada ya kukaushwa ikiwa umesagwa au bila kusagwa hutumika kama:
· Kiungo kwenye chakula na vitafunwa kama keki, mandazi,vitumbua
· Vikolezo kwenye vinjwaji km. chai, kahawa
· Dawa ya tumbo hasa wakati wa kuvimbiwa, kutoa hewa tumboni pia kuongeza hamu ya chakula
· Dawa ya ngozi

JINSI YA KUTUMIA
· kiungo kwenye chakula
Tumia maganda au saga magada yaliyokauka. Tumia ili kuongeza ladha kwenye vyakula kama pilau, ndizi, mchuzi nk
· Kutengenezea kinywaji
Weka vipanda vichache 2-3 (30gm) vya maganda kwenye kikombe ongeza maji yanayochemka, funika kwa dakika 15, ongeza vipande vya limao. Kunywa kila baada ya kula

MANUFAA
· Miti hudumu shambani zaidi ya miaka 20. Miti huchipua na kutoa machipukizi mengine kila baada ya kuvuna
· Gharama ndogo ya uzalishaji
· Mazao yaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu
· Magonjwa na wadudu ni kidogo
· Rahisi kuchanganya na mazao mengine
· Nguvu kidogo, kipato kikubwa.

FAIDA ZA KIAFYA ZA MAFUTA YA NYONYO


Habari yako msomaji,
Natumaini uko vema, unaendelea na kusaka mahela hapa duniani lakini usimsahau MUNGU katika kusaka na kutumia mahela.
Leo tuyakumbuke haya mafuta mazuri mno, ya nyonyo. Wengi tunaoyafahamu haya mafuta tunayajua kwa kazi yake kwenye kutatua tatizo la kutopata choo; yanafanya kazi vizuri tu nyanja hiyo.

Mafuta ya Nyonyo katika Kukuza Nywele


Mafuta ya nyonyo yanakuza nywele haraka, ukiyapasha joto kidogo kabla ya kupaka, kisha unapaka kwenye ngozi ya kichwa na kuyatawanya vizuri katika ngozi taratibu kama una massage kichwa chako pia bila kupasha kule kumassage kunayongezea joto linayoyapa uwezo wa kupenya vizuri. Unapopaka na kutawanya vizuri unasaidia kuongeza mzunguko wa damu kichwani hivyo virutubisho vinavyoletwa na damu kukuza nywele zako vinafika kwa utoshelevu.  Mafuta haya yana virutubisho mbali mbali ikiwemo Omega 6 fatty acids ambazo huongeza virutubisho vinavyoleta afya katika nywele zako.

Iwapo unataka utumie kama conditioner basi ukimaliza kupaka  kwenye ngozi paka katika ncha zako pia kisha vaa kikofia cha plastiki kisha baadae uzioshe nywele zako vizuri kuondoa mafuta kwa kuwa ulipaka mengi kama conditioner.
Mafuta ya nyonyo ni mazito sana, iwapo utaona una nywele nyepesi na hutaki ziligee kwa uzito wa mafuta pale unapopaka basi changanya na mafuta mengine hasa mafuta ya nazi kwa uwiano wa 1:1.


Mafuta ya nyonyo yanatibu mba na matatizo mengine ya ngozi ya kichwa.


Mafuta haya huwa na sifa ya kuwa na uwezo wa kuua bacteria na fangasi ambao huweza kuleta matatizo yanayosababishwa na vimelea hivi ikiwemo mba.
Iwapo una nywele kavu na una mba basi changanya mafuta ya nyonyo na ya mzaituni kidogo kisha paka kichwani pako kwa mfululizo mpaka shida yako ipungue au iishe.
Iwapo una mba na nywele zina mafuta mengi basi changanya hivi: kijiko kimoja kimoja cha mafuta ya nyonyo, asali na ute ute wa aloevera na maji ya nusu limao. Paka kwenye mizizi ya nywele yani kwenye ngozi kaa nayo dakika 30 kisha osha mchanganiko utoke kwenye nywele yako.
Pamoja na kutibu mba michanganyiko hii hurutubisha nywele na kufanya zing'ae.

Yanajaza nywele Zako

Mafuta ya nyonyo yana omega 6 na omega 9 acids ambazo ni virutubisho vinavyosaidia katika afya ya nywele yako. Ukitumia mara kwa mara mafuta ya nyonyo yanasaidia kuotesha nywele na kuzipa nguvu(kuzinenepesha) nywele zako ambazo tayari ni ndefu.


Unaweza kutumia kama conditioner 

Unapaka na kuvaa plastiki kisha unaosha, unaweza kulala nayo kichwani mpaka asubuhi. Pia unaweza kuchanganya na conditioner au steaming yako unayotumia.


Yanarudisha mng'ao wa nywele zako

Iwapo utayachanganyana mafuta mengine au utayatumia yenyewe yana virutubisho vinavyoiacha nywele yako iking'aa.

Iwapo unasumbuliwa na ncha za nywele zako hii ni dawa

paka mafuta ya nyonyo kabla ya kuosha nywele zako na shampoo, shampoo inamaliza baadhi ya mafuta ya asili kwenye nywele na kukupa ncha kavu zinazosababisha kuchomoka nywele zako unapochana.

Yanasadia kutibu chunusi

Haya mafuta yana kiungo chenye uwezo wa kuua bacteria wanaosababisha chunusi.


Pishana na uzee kwa mafuta ya nyonyo

Yanasaidia kuondoa vikunyanzi vidogo vidogo usoni vinavyotokea kwenye ngozi ya watu wenye umri mkubwa. Imeonekana mafuta haya ya kirutubisho kinachosadia kubalance collagen katika ngozi yako, collagen ndio kirutubisho kinachotunza ngozi ya ujana.

Kuza kope na nyusi kwa mafuta ya nyonyo

Inasemekana yamekuwa na mafanikio pia katika kukuza/kujaza kope na nyusi.

kupaka machoni


Upatikanaji wake

Mafuta ya nyonyo yapo yanayochujwa kwa njia ya kawaida kama ya nazi, mbegu za nyonyo hupondwa na kupikwa. Kuna haya maarufu kama 'Jamaican Castor Oil' haya huandaliwa kwa kukaanga kwanza zile mbegu kisha yanachujwa hivyo hutoka meusi. ni vema upate yaliyoandaliwa kiasili yasiwe super refined au yameongezewa kemikali.
mmea wake( mti wa nyonyo)
mbegu za nyonyo(castor beans/seeds)

our black Castor Oil
Jamaican Version

Tahadhali

Mafuta ya nyonyo yana harufu kali hivyo unaweza kuchanganya na kitu kingine kama mdalasini au mafuta mengine kupunguza harufu.

                                Jaribu uone haya mafuta yanavyofanya kazi.

                                     CREDIT : www.centilicious.blogspot.com